Fid Q feat Barakah The Prince - Mafanikio (Official Audio)

Опубликовано: 27 Июнь 2026
на канале: Fid Q
225,846
2.9k

#FidQ #Mafanikio #BarakahThePrince #SlideDigital

intro: Barakah The Prince
kila mtu anataka mafanikio..

verse 1:Fid Q
Kujisikia nipo juu mie sitaki hizo deals/
sipendi makuu hivyo nitabaki kuwa real../
na kila track ya Q aaah,.. ni wazi utaifeel/
ni wazi iko full aah MZAZI ninakill/
ninamwagika kama Masika../ ninaheshimika na sio kanjibai/
kwa huu mziki wa bajaji hadi kwa washkaji wenye macadillac/
unawashika ile kibabylon.. unauzika sana maghetoni/
ilimradi tu wawe happy more..midadi tu ila party noooo/
mkisinzia mtaniudhi nishawapa vyeo/
tuwape wapuuzi waliodai hii haiuzi haya matokeo/
safari ni hatua.. kufika inabidi uianze/
haina kukita au kusita.. inabidi ukaze/
ingia, ongoza au fuata njia, kukimbia ni mwiko/
kuanzia ulipo sio sawa na kubakia ulipo/
nikisema 'chini hapana' nina maana fanya unyanyuke/
na ukiamini umesimama mwana.. komaa usianguke/
ukijituma na neema inakaribia../
nyuma walio-give up mapema wangekaza wangeifikia/
penye... happy.. jitusu.. unafki usiuruhusu/
yajue ya kuzingatia ili uachane na yasiyokuhusu/
kibongobongo longolongo shazi/
endelea kusaka mchongo hata ukipata kazi/

HOOK: Barakah the prince
Tunachukiana? ndio../
ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio/
ongeza mbio/
sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio/
haukungoji wakati.. ooh wewe/
zinapita nyakati..ooh wewe/
muda wako bahati.. oh wewe/



verse 2:Fid Q
Na kughairisha kisa haupati sapoti/
ni kujificha na kuuliza giza.. iko wapi ile tochi?/
haupati ile noti/
na wakati wa ule uboss ushapotea/
hautaki ukose? usiache ofcoz endelea/
utafanikiwa kwa unachojua au unachofanya/
wachache ndio hutusua kwa jinsi tu wanavyoonekana/
mafanikio hayaji ukikata tamaa../
yenyewe huwafuata wanaojituma na wale wasiosukumwa na njaa/
sipigi kila dili mipaka imezingatiwa/
sitaki kuwa tajiri ninataka kufanikiwa/
ili kuheshimiwa kwanza ni lazima ujiheshimu/
lakini kufanikiwa ni maujanja tu sio lazima elimu/
ili kuyadaka wengine hugeuka wabaya/
mafanikio kwenye kuyasaka wengine hugeuka malaya/
hugeuka was(i)o haya/
kutwa utawakuta kwa babu/
na anayefanya mambo ya maana huwa hana muda wa kuyahesabu/
kwenye kuyasaka hakikisha haufilisiki/
haupotezi maisha au vile vitu havinunuliki/
sio kama hatucheki kwasababu tumezeeka?/
nope.. ni tunazeeka kwasababu hatujawahi cheka/

HOOK: Barakah the prince
Tunachukiana? ndio../
ila sio sababu kuacha riadha ya mafanikio/
ongeza mbio/
sababu kila mtu, kila kona anasaka mafanikio/
haukungoji wakati.. ooh wewe/
zinapita nyakati..ooh wewe/
muda wako bahati.. oh wewe/
utumie basi... eeeh eeeh/

bridge: Barakah The Prince
una mpenzi (na) uko lonely?/
im sorry ndugu.. haujafanikiwa/
maisha ni kama boli, magoli ndio kufanikiwa/

oooh ooh oooh..oooh.. ndio kufanikiwa/
kila mtu anataka mafanikio.../

outro:Barakah The Prince
hhhmmm.. hhhhmmm.. oh mafanikio
oh mafanikio
kila mtu anataka mafanikio

FID Q Songs OUT WORLDWIDE ON MAJOR DIGITAL STORES:

Written & Performed by Fid Q

Follow Fid Q on
Twitter:   / fidq  
Facebook:   / fidhop  
Instagram:   / therealfidq  

Channel Administered by Slide Digital
Instagram: www.instagram.com/slidedigitaltz