#NduatiMurigi #Chunga #NgommaGospel
Lyrics
[Verse 1]
Straightthrough me nakam na machungu
Ju ya vile hawa watu wanachezea Mungu
Brikicho, guess what? Mmeshaua nyungu
Na ndio Huyo kwa corner anakuja na rungu
Ye ndio aliumba kila kitu unaonanga
Usiku mchana, wadudu wanyama
Viumbe vyote vikimwona huwa vinainama
But sisi tunam-assume ka huduma namba
Sasa vijana wote kazi ni kubet
Ka si kubet pombe wanamaliza crate
At this rate for sure si tutaregret
Si secret ii taifa si inaneed help
Watoto wanaimba wanataka lamba paka
Boychild kukataliwa anaitana takataka
Mnadhani mnaweza fanya tu kenye mnataka
Chunga, kiboko yenu ni mafuta inapakwa
[Hook]
Chunga! Kiboko yenu ni mafuta inapakwa.
Chunga! Chunga! Kiboko yenu ni mafuta inapakwa.
[Verse 2]
Hawa wanasiasa aki wana siasa
Wengi walipewa kazi na hawajai anza
Wanainsist kuitwa waheshimiwa kila stanza
Hawajui wanaact kama vijana kwa vinyasa
Wanapenda pesa za kuiba
Kukula wanakula na hawajawai shiba
Sasa wanazidi kutuweka kwa msiba
Ju ya ulafi wa pesa na kutojali taifa
Housing allowance wamejiongeza mamita
Roysambu ni bedsitter zimejaa bed sita
Wasichana wetu wadogo mmeanza kuwaita
No wonder mnapunguza umri iwe kumi na sita
Mungu anaona kila kitu mnafanya
Hata iwe kwa giza ataleta kwa mwangaza
Mlipewa kura mkajiona wajanja
Chunga, kiboko yenu ni mafuta inapakwa
[Hook]
[Verse 3]
Mapastor fake kule S.A na Malawi
Hakuna fruits, wanainsist kutuonyesha matawi
Kulenga word kuinsist na power,
Niambie iko wapi tofauti yenu na wachawi?
Na hawako mbali, wamepenya hadi Kenya
Kile wanahubiri si kile Mungu alisema
Kupotosha umati, kufanya vituko
Wanajua msisimko itanyonya mifuko
Ni rahisi kupoint fingers alafu usahau:
"Wow, me ni kama wao.
Ni mara thao nimefanyia God madharau
Unawonder now, utajiokoa how?"
Suluhu ni simple, kukiri na kutubu
Kubadilisha njia na kumlilia Mungu
Siku ya kiama kila mtu atapatwa
Usipochunga ata yako ni mafuta inapakwa
[Hook]
Free download: https://bit.ly/2HtMOQM
#Chunga #KovuChallenge