Makundi tofauti yameendelea kutoa mapendekezo yao mbele ya kamati ya maridhiano. Aliyekuwa mwanasheria mkuu Githu Muigai, ametaka kupunguzwa kwa maeneo bunge na kaunti akisema kwamba wabunge ni wengi mno. Pia muigai alikosoa mapendekezo ya kuongeza idadi ya maeneo bunge akisema ni mzigo mzito kwa mlipa ushuru.