SERIKALI imebainisha kuwa watumishi wanakumbana na changamoto nyingi zinazo walazimisha kuhama kutoka eneo moja kwenda lingine hasa wanandoa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora George Simbachawene ametoa kauli hiyo leo Juni 8 2023 bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali na majibu ambapo amesema kuwa watumishi wa namna hiyo hawawezi kufanya kazi kwa ufanisi kwasababu muda mwingi wanafirikia juu ya wenza wao kuwa mbali.