105 - Mchungaji Mpenzi "Jesus The Loving Shepherd"

Опубликовано: 05 Август 2026
на канале: Victory S.D.A Church Kisumu
168
4

105 - Mchungaji Mpenzi
"Jesus The Loving Shepherd"


1
Mchungaji mpenzi hukuita uje
Katika zizi lake panapo salama;
Akina wanawake, waume vijana,
Yesu aliye kweli, huwaita kwake.

Chorus
Huita kwa moyo wa huruma, "Uliyepotea uje kwangu"
Hivi kukungoja anadumu, Bwana Yesu Mchunga.

2
Akatoa maisha kwa ajili yetu;
Ataka wapotevu waje kwake sasa;
Tusijihatirishe; Kwake tu salama;
Sikia wito wake, Mchungaji wetu.

3
Tusikawie tena, adui Shetani,
Kama mbwa wa mwitu, atatuharibu;
Tunaitwa na Yesu, Mkombozi wetu,
Tuingie zizini, panapo nafasi.