Hatifungani ya Stawi yenye thamani ya Shilingi Bilioni 150 ambapo kwa awamu ya kwanza itatumika bilioni 50 , ikiwa ni mpango wa miaka mitano wa kuingia soko la mitaji kwa mara ya kwanza nchini.
Hatifungani hii inalipa riba ya asilimia 13.5 kwa mwaka, na itasaidia kutoa mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati ili kukuza biashara zao na kukuza uchumi wa taifa.
Katika uzinduzi huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Mkurugenzi Mtendaji wa TCB na Afisa Mtendaji Mkuu wa CMSA walisisitiza umuhimu wa hatifungani hii katika kupanua masoko ya mitaji na kupunguza utegemezi wa mikopo kutoka nje.
Tazama video hii kujua zaidi kuhusu fursa hii mpya ya uwekezaji na mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati nchini Tanzania.
#TCB #MikopoNafuu #MasokoYaMitaji #Wajasiriamali #Stawi #Tanzania