Msamiati wa jikoni
Jiko – chombo cha kupikia. Jiko linaweza kuwa la makaa, kuni, stima, mvuke, gesi na hata la jua.
Seredani – jiko la makaa.
Mafiga/mafya – mawe matatu ya jiko la kuni.
Dohani – mfereji wa kutolea moshi jikoni.
Karo – sehemu ya jikoni ya kuoshea vyombo.
Mwiku/kiporo/ bariyo/uporo – chakula kilicholala mpaka asubuhi.
Ukoko – mabaki/ masazi ya chakula yanayoganda kwenye chombo kilichopikia chakula hicho.
Staftahi – kifunguakinywa
Kisabeho – chakula cha asubuhi.
Kishuka/ chamcha – maakuli ya adhuhuri
Kilalio/chajio – chakula cha jioni
Masizi – unga mweusi wa makaa au moshi ambao aghalabu hupatikana kwenye sufuria au chungu cha kupikia.