MALALAMIKO YA UANDIKISHAJI WILAYA YA KARATU | UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.!!

Опубликовано: 27 Сентябрь 2026
на канале: Swahili Villa Online TV | Washington, D.C
128
1

Anasema mtoa taarifa kwamba huyu Msimamizi wa Kituo anaitwa Mussa ni Mratibu wa Elimu Kata ya Qurus Wilaya ya Karatu toka siku ya kwanza tulianza kuona kasoro Mbalimbali kama kuandika Majina ya watu ambao hawajafika vituoni hatujui majina anatoa wapi tukimuuliza anatuambia ni Majina ya Watumishi waliopo kwenye kazi tukamuuliza kanuni inaruhusu?

Akatuomba radhi hiyo siku aliwaandikisha watu 3 lakini baada ya hapo tuliona kasoro nyingi hasa baada ya kuona idadi ya watu imepanda sana yaani watu wanaweza kuja 70 kituoni lakini jioni idadi inaenda karibu hadi 150 kumbe jamaa anaruka kurasa za Daftari ili usiku akajaze majina anayejua yeye wengine ameandikisha majina mawili tu kwa shida ni Kubwa tukihoji haya Mambo tunaonekana tunafanya vurugu vituoni Uchaguzi huu umeanza kuvurugwa Mapema.