Katibu Mkuu wa Umoja wa wazazi Jumuiya ya CCM Taifa Ally Hapi amewasili Wilaya ya Bagamoyo ikiwa ni katika mwendelezo wa Ziara yake ya siku nne mkoani Pwani yenye lengo la Kuimarisha Jumuiya ya Wazazi na chama cha mapinduzi katika Mkoa wa Pwani.
Hapi aliyeambatana na Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya hiyo Aza January Joseph wamepokelewa na wanachama na viongozi mbalimbali wa chama pamoja na wabunge wa majimbo ya Bagamoyo na Chalinze ambapo baada ya kuwasili katika Ofisi za Chama wilaya ya Bagamoyo Hapi alipokea taarifa ya uhai wa chama na jumuiya zake na baadae kufanya mazungumzo na wanachama waliojitokeza katika eneo la mapokezi