KUWA NA YESU MWOKOZI
1. Yesu Mwokozi, kwa hakika, Hunipa furaha na amani;
Mrithi wa wokovu wake, Natakaswa kwa damu yake.
Chorus
Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu.
Habari hiyo wimbo wangu, Daima nitamsifu Yesu.
2. Nijitoapo nina raha, Na kwa imani namwona Bwana;
Aniletea malaika, Wananilinda, niiokoke.
3. Hali na mali anitwaa, Katika Yesu nabarikiwa;
Nikimgoja kwa subira, Wema wake unanitosha.
Blessings.
#breathofpraise #hymns #gospel