Semina ya amani iliyofanyika KMT Nyabange, Musoma, ambapo washiriki takriban 50 kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania walishiriki wakiwakilisha Dayosisi za KMT, wakiwepo Maaskofu 3, Wachungaji, Mashemasi, Viongozi wengine wa Kanisa na Wataalam mbalimbali pamoja na Waumini. Semina ilifanyika kuanzia tarehr 26 hadi 29 Machi 2024 katika Chuo cha Theolojia kinachoitwa MTCEA.
Maazimio kafha wa kadha yalifanyika, ikiwa ni pamoja na kuunda uongozi na kuandaa mpango mkakati wa kuiendeleza shughuli ya amani katika KMT.
Hata hivyo, wanasemina walipendekeza kwamba, ili shughuli za amani zifanyike kwa ufanisi ni wakati sasa kuwe na chombo rasmi kama zilivyo idara ndani ya Kanisa kitakachotambuliwa katika mfumo wa Kanisa (Katiba, Kanuni na Miongozo) na ndipo kazi hii itafanyika kwa uhakika na kwa urahisi.