Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania anatangaza nafasi za ajira kwa vijana
wenye elimu ya Shahada, Stashahada, Astashahada, Kidato cha sita na
Kidato cha nne.
download pdf here 👇👇👇
https://shorturl.at/lwDQ1
1. Sifa za Muombaji
a) Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa.
b) Awe amehitimu kidato cha nne au sita kuanzia mwaka 2018 hadi 2023.
c) Kwa waombaji wa kidato cha nne na sita pamoja na wenye Astashahada
wawe na umri kuanzia miaka 18 hadi 25.
d) Kwa waombaji wa kidato cha nne wawe na ufaulu wa daraja la kwanza
mpaka la nne (Division I – IV). Kwa waombaji wenye ufaulu wa daraja la
nne (Division IV) wawe na ufaulu wa alama (Point) 26 hadi 28.
e) Kwa waombaji wa kidato cha sita wawe na ufaulu wa daraja la kwanza
mpaka la tatu (Division I – III)
f) Wahitimu wa Shahada na Stashahada wawe na umri kuanzia miaka 18
hadi 30.
g) Awe na urefu usiopunguwa futi tano na inchi nane (5’8”) kwa wanaume, na
futi tano inchi nne (5’4”) kwa wanawake.
h) Awe na kitambulisho cha taifa au namba ya utambulisho kutoka mamlaka
ya vitambulisho vya taifa (NIDA).
i) Awe na uwezo wa kuongea lugha ya Kiswahili na Kingereza.
j) Awe na afya njema kimwili na kiakili iliyothibitishwa na daktari wa Serikali.
k) Awe hajaoa/kuolewa au kuwa na mtoto.
l) Awe hajawahi kutumia dawa za kulevya.
m) Awe tayari kuhudhuria mafunzo ya awali ya taaluma ya Polisi.
n) Awe hajaajiriwa au hajawahi kuajiriwa na taasisi nyingine ya Serikali.
o) Awe tayari kufanya kazi za Polisi mahali popote Tanzania.
p) Awe tayari kujigharamia katika hatua zote za usaili endapo ataitwa kwenye
usaili.
q) Asiwe na alama za kuchorwa mwilini (tattoo).
r) Asiwe na kumbukumbu za uhalifu.
s) Kwa waombaji wenye elimu ya kiwango cha Shahada (NTA level 8),
Stashahada (NTA level 6) na Astashahada (NTA Level 5 au NVA Level 3)
wanatakiwa wawe na fani zilizoainishwa kwenye tangazo hili.
2.Utaratibu wa kutuma Maombi
1. Waombaji wote wanatakiwa waandike barua za maombi wao wenyewe kwa
mkono (Handwriting) bila kusahau namba za simu na watumie anuani ya
Mkuu wa Jeshi la Polisi S.L.P 961 DODOMA.
2. Waombaji wote wafanye maombi yao kupitia kwenye mfumo wa Ajira wa
Polisi (TANZANIA POLICE FORCE – RECRUITMENT PORTAL)
unaopatikana kwenye tovuti ya Jeshi la Polisi www.polisi.go.tz
3. Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 16/05/2024.
#ajira
#polisi
#jeshilapolisi
#ajira2024
#ajirampya
#governmentjobopportunities
#tanzania