LATRA yafanya Ukaguzi wa Mwaka kwa Reli ya Kati (MGR)

Опубликовано: 05 Октябрь 2026
на канале: LatraTV
638
5

Mha. Hanya Mbawala Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Reli Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA), amefanya ukaguzi wa usalama wa reli kwa reli ya kati kuanzia Tabora hadi Mpanda Mkoani Katavi kuanzia Septemba 24 hadi Octoba 03, 2024.

Ukaguzi huo umelenga kukagua reli yenyewe (njia ya treni), Mabehewa ya Treni pamoja na usalama wa reli kwa ujumla.

Mha. Mbawala ameambatana na Bw. Bahati Shagihilu Afisa Usafirishaji Wizara ya Uchukuzi, Mha. David Matiko Kutoka Shirika la Reli Tanzania (TRC), pamoja na Mha. Medani Ndabagoye na Mha. Micheal Mwachiko Maafisa Wakaguzi wa Reli kutoka LATRA.