Tunaona visa vingi sana vya Curtis Jackson (50cent) kwenye mitandao ya kijamii na movies pia.. kama nilivyokupa intro kwenye video, lakini je Umewahi kujua ni mambo gani amepitia huko nyuma?.
Kifo cha mama yake.
Uuzaji wa dawa za kulevya
Nyimbo ilivyopelekea kifo cha DJ JAM hadi 50 kupigwa risasi 9
Na kubambikiwa kesi???... tushuke na thread
NO 1
Mama yake Aliuawa kwasababu ya biashara ya madawa ya kulevya.
Mama wa 50 Cent alifariki na kumuacha mtoto Curtis akiwa na miaka 8 mtoto asiyemjua baba toka azaliwe, so sad. Curtis Jackson AKA 50 CENT , anamsimulia mama yake kama mwanamke shupavu na mgumu kinomanoma. Curtis alipotoka shule akiwa amepigwa na wenzake, ushauri wa mama yake ulikua – acha kulia lia, okota chochote kilicho karibu yako umpige aliye kuchokoza. Anasema maisha haya ndio chanzo cha kifo cha mama yake, aliwekewa kitu kwenye kinywaji na kufunguliwa hewa chafu ya sumu hivyo kupelekea kifo chake. Curtis (50cent) anasema, kwa jinsi watu wanavyomzingua, angepata malezi ya mama hadi ukubwani basi asingekuwa hivi leo hii; ANGEKUA AMEPATA KESI ZAMANI SANA.
NO 2
Alifuata nyayo za mama yake kwa kuuza unga.
Ronald Reagan era, kama anavyoukashifu huu mwaka Kendick Lamar na Kama ilivyo kwa wasanii wengine wengi wa hiphop, 50 alifanya biashara ya madawa ya kulevya akiwa mdogo sana., 50 akiwa na miaka 12 mwaka 1980 alishaanza kuuza unga na kufuata nyayo za mama yake. Alifanya shughuli hiyo kwa muda mpaka akawa mtaarishaji wa unga, anajua kuuchemsha hadi kuugandisha na kuuza.
NO 3
Anahusishwa na kifo cha Jam Master Jay's dj, NA NDIO SABABU ya kisa number 4
Jam Master (Jason Mizell) aligundua kipaji cha 50 huko mtaani na kumpa shavu la kurecord album. Nyimbo mojawapo katika ile album iliitwa “GHETO QURAN” , hii nyimbo alizungumzia maisha yake ya mtaani wakati anasambaza madawa na kuwataja baadhi ya watu ambao walikua ndio madon wa hii kazi, lilikua kosa kubwa sana. 50 alipigwa marufuku kurecord studio lakini Mizel aliinga hili suala na kuforce dogo aendelee kurecord, siku chache baadae Mizel aliuawa. Kesi ilinguruma mpaka mwaka 2017 na kupuuzwa.
NO 4
50 alipigwa risasi 9 akiwa mtaani karibu na nyumbani kwa bibi yake.
Album iliyopigwa marufuku kutoka studio HAIKUTOKA, na siku kadhaa mbele, 50 alishambuliwa na watu waliokuwa kwenye gari akiwa maeneo ya mtaani kwao (alipokulia, kwa bibi). Alipigwa risasi ya mkono, bega, paja, miguu yote miwili, kifua na shavu la kushoto na kumkata ulimi, kovu ambalo linaonekana mpaka leo hii. Sababu ni ile ile album na nyimbo ya Gheto Quran , kuna mstari alimtaja jambazi na zungu la unga Kenneth "Supreme" McGriff, naye akatoa oda 50 auawe. Kupitia many man 50 anasema aliyempiga risasi alikufa siku chache baadae na waliomtuma wangojee kisasi hiko hiko.
N0 5.
NYPD Walitaka kumbambikia kesi
Polisi walitaka kujua nyendo za 50 na walimlazimisha marehemu rapa Prodigy (kutoka Mobb Deep) kumuwekea bunduki 50 kwenye gari lake ili waweze kumkamata. P hakufanya hivyo, bali alimweleza 50 mchongo wote unayokwenda.
Hii alisimulia 50 mwaka 2017 baada ya P kufariki kwa ugonjwa Siko Sel (sickle cell anaemia)