Bado tupo kwenye majanga, watu wamepitia mambo bwana. leo tumcheki mkali wa movie ya The Matrix na John Wick, KEANU REEVES ambaye ni Raia wa Canada. Huyu jamaa ni maarufu kwa kuishi kawaida tofauti na watu wote maarufu. Sio tajiri na hashitui, amewahi kutoa asilimia 70 ya mshahara wake wa movie ya The Matrix kwaajili ya wagonjwa wa Leukemia. Ametoa na anatoa misaada mingi bila kujitangaza.
Ni mzaliwa Wa Beirut Lebanon akiwa na mama muingereza na baba mchina wa hawaii (Usishangae wachina kupatikana hawaii, walikwenda kushughulika karne ya 19, wengine ni Samoans ambao wengi asili yao ni philipino RIP UMAGA) tusikeshe hapa, tuendelee na Keanu.
Watu walisema baba wa keanu aliwaacha akiwa na miaka mi 2
Wengine mi 3 lakini baba mzazi alikiri kutengana na familia Keanu akiwa na miaka mi 5. Alijitokeza mara kadhaa mpaka Keanu alipotimiza miaka 13, hapo alipotea mazima miaka 10 bila salamu wala barua.
Hii ilimfanya keanu kutomaliza hata diploma alipokua highschool, kwa mawazo alisumbuliwa na matatizo ya kutoshika akilini mafunzo ya darasani (Dyslexia) hapo alishahama shule kama 4 kwa miaka mi 5.
Pigo la Pili
Akiwa tayari amezama kwenye tasnia ya Filamu. Alimpoteza muigizaji na rafiki yake kipenzi River Phoenix kwasababu ya dawa za kulevya (Drug overdose) Phoenix akiwa na miaka 23.
Pigo la tatu lenye utatu mzito.
Mwaka 1999 akiwa na mpenzi wake Jennifer Syme, walimpoteza mtoto wao ambaye alifariki baada ya kuzaliwa njiti.