UNAWEZA KUPATA UJAUZITO UKIWA BADO UNANYONYESHA

Опубликовано: 18 Сентябрь 2026
на канале: WikiElimu
1,497
4

#Dr_Mniko #wikielimu
Mwanamke anaponyonyesha, mwili wake unatoa homoni inayoitwa prolactin, ambayo inasaidia kutoa maziwa na inasaidia pia kuzuia yai la uzazi kutolewa.
Kwa sababu inazuia yai kutolewa, inaweza kupunguza uwezekano wa kushika mimba, lakini hii haina maana haiwezekani.
Ili usipate mimba unaponyonyesha yapo masharti unayopaswa kutimiza,
1. Inafaa katika kipindi cha miezi 6 ya mwanzo pekee, kipindi ambacho mtoto ananyonya maziwa ya mama pekee.
2. Nyonyesha mtoto kila anapohitaji usiku na mchana na hakikisha haukai muda mrefu bila kumyonyesha
3. Hakikisha damu ya hedhi haijanza kutoka, kama imeanza tumia njia nyingine kupanga uzazi