SUKARI INASABISHA KANSA?

Опубликовано: 14 Июль 2026
на канале: WikiElimu
223
3

#Dr_Mniko #wikielimu
Moja ya dhana inayosambaa katika mitando mingi ya kijamii ni ile inayosema mtu mwenye saratani asile sukari kwa sababu inaenda kusababisha seli za kansa kukua haraka na kusambaa zaidi mwilini. Hii si kweli. Mwili wako unahitaji sukari.
Seli zote mwilini zinahitaji nishati ili kuendelea kuishi na kufanya kazi.
Na zinapata nishati hii kupitia aina ya sukari inayoitwa glukosi. Glukosi ndio chanzo cha nishati kwa seli zote mwilini, sio tu kwa seli za kansa.
Sukari inapatikana kwenye vyakula vingi tunavyokula, matunda, mbogamboga, nafaka, na bidhaa za maziwa.
Ukila mwili unameng’enya chakula na kutengeneza glukosi ambayo inatumiwa na seli zote mwilini
Nikwambie tu, kula sukari pekee hakusababishi mtu kuwa na saratani.