Mara nyingi tunasikia kwenye television na kwenye radio kuwa ni muhimu kunywa maziwa ili kuwa na mifupa imara na kuzuia matatizo ya kufubaa kwa mifupa. Je, hii si kweli
Mifupa inahitaji virutubisho mbalimbali, madini ya calcium, vitamini D, Vitamini K, na protini ili kuwa imara.
Aina zote hizi za virutubishi zinapatikana ndani ya mlo kamili, ambao unahusisha vyakula aina nyingi, na sio maziwa pekee.
Madini ya calcium kwa mfano, yanapatikana pia ndani ya vyakula kama yogurt, jibini, mbogamboga kama spinach, dagaa, maharage,na mbegu za mlozi
Lakini pia, kukaa kwenye jua kunasaidia kutengeneza vitamin D ambayo ni kirutubishi muhimu kwa afya ya mifupa.
Mazoezi ya mara kwa mara, kama vile kutembea, kubeba vitu vizito, pia husaidia kuwa na mifupa imara.