MTOTO AKIMEZA SHILINGI INATOKA LINI?

Опубликовано: 14 Июль 2026
на канале: WikiElimu
164
4

Ni imani mbayo imekuwepo kwa watu wengi kwa miaka mingi, kuwa, ukimeza shilingi au kitu kinginge chochote kidogo, inachukua mpaka miaka 7 kutoka. Lakini hii si kweli.
Mfumo wa kumeng’enya chakula umeundwa kwa ajili ya kuchakata, kuvunjavunja na kunyonya virutubishi kutoka kwenye chakula tunachokula.
Unapomeza kitu kama shilingi, inafuata mfumo huu huu.
Kwa kawaida, unapokula chakula,kinasafiri kutoka kwenye umio mpaka kwenye tumbo, hapa kitakutana na kitavunjwa vunjwa na asidi za tumboni.
Baada ya hapo kitaingia kwenye utumbo mdogo, na hapa virutubishi vitafyonzwa kuingia kwenye mfumo wa damu.