Wapo watu wengi wanaamini kuwa kuvaa chupi, boxer au tight inayobana sana, inaongeza joto kwenye korodani na hii inaweza kusababisha kupungua kwa kiasi cha mbegu za kiume kinachotengenezwa na kupunguza urijali wa mwanaume.
Lakini ukweli ni kuwa, hakuna ushaidi wa kutosha wa kisayansi kusema kuwa dhana hii ni ukweli.
Ni kweli kwamba, joto la kwenye korodani ni dogo ukilinganisha na mwili, na inaaminika kwamba joto likiwa chini inasaidia mbegu za kiume kutengenezwa kwa wingi. Na ndio maana, pumbu zinaning’inia chini kidogo ya mwili.
Ni ukweli kwamba, baadhi ya tafiti zimeonesha kwamba mtu akivaa chupi ambayo inabana sana, inaongeza joto kwenye korodani na kupunguza ubora wa mbegu zinazotengezwa.
Lakini, athari hii ni ndogo na haionekani kwamba inaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kiasi hicho mpaka kusababisha ugumba