#Dr_Mniko #Wikielimu anazungumza kuhusu sukari na ugonjwa wa kisukari
Ugonjwa wa kisukari ni tatizo la kimetaboliki linalosababishwa kuwepo na kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu.
Kuna aina mbili za ugonjwa wa kisukari: aina ya 1 na aina ya 2.
Aina ya 1 inasababishwa na kuzaliwa na mfumo wa kinga unaoharibu seli za kongosho na hivyo kupelekea upungufu wa homoni ya insulini ambayo ni muhimu katika kudhibiti sukari mwilini.
Kwa hiyo, kisukari aina ya 1 haisababishwi kwa kula sukari, bali kwa kukosa homoni ya insulin, ambayo inatokana na kuharibiwa kwa seli za kongosho