Ni kweli, wengi wetu kwa wakati fulani tumewahi kujaribu kupaka dawa ya mswaki kwenye jeraha baada ya kuungua. Hii ni Imani ya watu wengi.
Lakini ukweli ni kuwa, kupaka dawa ya mswaki hakusaidii na wala hakupendekezwi.
Baada tu ya kuungua, njia bora zaidi ya kujitibu ni kuweka sehemu iliyopungua ndani maji yanayotiririka kwa dakila 10 mpaka 20 ili papoe.
Kuipooza sehemu iliyoungua inasaidia kupunguza maumivu, kuzuia moto kuchoma zaidi na kusaidia mchakato wa kupona kuanza.
Lakini, usitumie maji ya barafu au baridi sana, yanaweza kusababisha shida zaidi kwenye ngozi ambayo tayari imeungua.